Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura yaanza kutoa leseni ujazaji gesi asilia

6b5488cfb35d7cb6208a7178fade4cb2 Ewura yaanza kutoa leseni ujazaji gesi asilia

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imeanza ukaguzi na utoaji Leseni kwa wafanyabiashara binafsi wanaotaka kujenga vituo vya kujaza gesi kama ilivyo kwa mafuta.

Katika mchakato huo, ujenzi unatarajia kuchukua mwezi ukijikita kuhakikisha usalama wa wananchi maeneo wanayojenga vituo hivyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Gesi Asilia wa Ewura, Thobias Rwelamila, alisema kampuni binafsi 24 zilitaka kufanya biashara hiyo na mchakato ulichelewa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona lakini sasa wameanza kutoa leseni.

“Kuna kampuni moja ambayo imefika Ewura n kufanya ukaguzi maeneo anayotaka kujenga kuhakikisha usalama wa wananchi, vibali za ardhi, mazingira na vingine muhimu,” alisema.

Alieleza ili kuharakisha utoaji leseni watatumia njia za kawaida za uchambuzi wa maombi. Alisema kampuni zenye nia ya kufanya biashara hiyo zitaanza mchakato wa kupatiwa leseni kuwezesha kuanza ujenzi kwa kufuata utaratibu.

Meneja Biashara ya Gesi wa TPDC, Emmanuel Gilbert alisema baada ya bodi ya shirika hilo, kutoa idhini ya kampuni binafsi kwa biashara hiyo, kampuni zinazohitaji zinapaswa kupeleka maombi maalum ili zipatiwe idhini Ewura.

“Gesi inatakiwa kuuzwa kwa bei isiyomnyonya mtumiaji na mfanyabiashara apate faida kwa kuhakikisha vituo vina viwango kuepuka milipuko lazima kubanwa na Ewura,” alisema.

“Baada ya kupatiwa leseni na Ewura, wataanza ujenzi miezi sita ya uagizaji vifaa vya ujenzi na baadaye ujenzi, kwani vifaa hivyo unaagiza ndio unatengenezewa, hivyo tunatarajia Februari mwakani ujenzi utaanza,” alisema.

Katika makadirio ya awali kabla ya corona,Mei 30, mwakani ujenzi wa vituo hivyo utakuwa umekamilika na kama hakuna changamoto, vitaanza kutoa huduma ya kuuza gesi asilia kwa ajili ya magari na matumizi mengine nchini.

Alisema mradi huo unaenda na ujenzi wa vituo vikubwa viwili (Mother station ) vya kujaza mafuta Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Ubungo katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani cha sasa kujaza gesi kwenye mabasi ya Mwendokasi, ambayo yatatumia gesi asilia.

Chanzo: habarileo.co.tz