Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura: Tatizo la mafuta sio Tanzania pekee

Mafuta Mjadala Ewura: Tatizo la mafuta sio Tanzania pekee

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura CCC) limesisitiza kuwa tatizo la uhaba wa mafuta halipo Tanzania peke yake bali linaikabili dunia nzima.

Akizungumza na Mwananchi kwenye banda la maonyesho ya 29 ya wakulima Nanenane Agosti 8, 2022, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Mhandisi Goodluck Mmari amesema kuwa changamoto ya uhaba wa mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa ni mtambuka ambalo limechangia na vita katika baadhi ya mataifa.

"Tunatarajia vita hivyo vikikoma hali ya upatikanaji wa mafuta inaimarika hivyo tuvumilie na tunaomba Watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito'' amesema.

Amesema kuwa wanatambua changamoto inayowakumba Watanzania hususan wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kutokana na hali hiyo kama Serikali inaendelea kuangalia namba ya kuondoa athari hiyo kwa watanzania.

SOMA:Bei ya mafuta yazidi kupaa Tanzania

Makamu Mwenyekiti wa Ewura-CCC, Anna Mungai amesema baraza hilo linatumia fursa ya maonyesho ya nanenane ya mwaka huu kuwahimiza watoa huduma zinazodhibitiwa na Ewura, kuhakikisha huduma zinakuwa za uhakika.

Related Bei ya mafuta yazidi kupaa TanzaniaAdvertisement "Tunawakumbusha watoa huduma za nishati na maji uhakika wa upatikanaji wa huduma hizo na kwa gharama nafuu wanazoweza kumudu Watanzania wengi, katika kufikia ajenda ya 10/30 ambayo inakitaka kilimo kuwa biashara" alisema.

Dereva bajaji, Julius Amoni amesema ni wakati Serikali kuangalia namna bora ya kusaidia sekta ya usafirishaji na kilimo kuondokana na adha ya kupanda na kushuka kwa nishati ya mafuta nchini.

''Sekta hizo zinategemeana unapokuta mafuta yanapanda na usafiri unapanda kwa watanzania mpaka sasa tuna fika wakati kuhusisha hali hiyo na mambo ya kisiasa licha ya vita ya Russiaā€¯

Chanzo: Mwananchi