Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elon Musk kuhakiki watumiaji wa Twitter

Elon Mask111.png Elon Musk

Fri, 29 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tajiri namba moja duniani Elon Musk ana mpango wa kufanya uhakiki wa watumiaji wote wa mtandao wa Twitter ili kuthibitisha wale ambao ni binadamu.

Musk ameyasema hayo wakati akiendelea na mipango ya namna atakavyouendesha mtandao huo mara baada ya kuununua rasmi.

Mpango huo umewaacha wengi wakishangaa na kujiuliza bila kupata majibu ni namna gani haswa mfanyabiashara huyo anataka kuubadili mtandao huo.

Baadhi ya mambo ambayo wataalamu wameanza kufikiria ni kuwa Musk anaweza akahitaji watumiaji wote wa Twitter kutumia majina yao ya kweli kwenye akaunti zao au anaweza akaendelea kuruhusu majina bandia.

Elon amesema anaweza akatafuta kampuni ya pembeni ili imsaidie kukusanya picha ya ukweli kama kitambulisho cha kila mtumiaji wa Twitter ama pia anaweza fanya ushirikiano na kampuni zingine ambazo watumiaji hao tayari wanajulikana.

Kutegemeana na matokeo ya mipango yake, kuna uwezekano mkubwa wa kuja kutokea mabadiliko makubwa kwa mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live