Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elon Musk amfuta kazi mfanyakazi aliyemkosoa

Elon Musk Auza Hisa Za Thamani Ya Dola Takriban Bilioni 4 Za Tesla Elon Musk amfuta kazi mfanyakazi aliyemkosoa

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmiliki wa Twitter, Elon Musk aliingia kwenye mzozo na Mhandisi wa programu za Kompyuta kwenye mtandao wa Twitter hali iliyopelekea Bosi huyo wa Twitter kutweet “amefutwa kazi” lakini Mhandisi huyo alithibitisha kuwa alipoteza mawasiliano na mfumo wa ndani wa Twitter.

Kwa mujibu wa ripoti tajiri huyo namba moja Duniani aligombana hadharani na idadi kubwa ya waajiriwa wa mtandao huo juu ya mwenendo wake ikiwemo kumfuta kazi Mhandisi Eric Frohnhoefer hadharani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Frohnhoefer kuthibitisha kuwa Musk alikosea juu ya madai kwamba Twitter ilikuwa ikiendeshwa kutokana na maneno ya Bilionea huyo.

Inaelezwa kuwa siku ya Jumanne idadi kubwa ya waajiriwa wa kampuni hiyo walifutwa kazi kwa kutumia ujumbe kupitia email uliosomeka “tabia yako imekiuka sera za kampuni”

Vyanzo vimeiambia CNN kwamba wafanyakazi katika siku za hivi karibuni walikuwa wazi sana kumkosoa Musk katika Slack ya kampuni. (CNN imejaribu kuwasiliana na wafanyakazi waliofutwa kazi ili kuthibitisha.

Akijibu juu ya tweet juu ya taarifa ya kuwafuta kazi waajiriwa hao siku ya Jumanne Musk alisema:- “Ningependa kuomba radhi kwa kuwafuta kazi hawa wataalamu. Talanta zao zisizo na kipimo zitakuwa na manufaa kwingineko.”

Kufuatia hatua hiyo, Musk sasa anaendesha Twitter kwa usaidizi wa marafiki zake Jason Calacanis na David Sacks pamoja na wakili wake binafsi Alex Spiro.

Inaelezwa pia kuwa anawatumia wahandisi kwa mkopo kutoka kwa baadhi ya makampuni yake mengine, ikiwa ni pamoja na Tesla (TSLA).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live