Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elon Musk agoma kujiunga bodi ya Twitter

Elon Musk Twiiterrrr Elon Musk agoma kujiunga bodi ya Twitter

Mon, 11 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Elon Musk ameamua kutojiunga na bodi ya Twitter, afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Parag Agrawal anasema.

Uteuzi wa Bw Musk ulipaswa kuanza kutekelezwa Jumamosi baada ya kufichua wiki jana kwamba alikuwa amenunua asilimia 9.2 ya hisa katika mtandao wa kijamii.

Hata hivyo, Bw Agrawal aliandika: "Elon alishiriki asubuhi hiyo hiyo kwamba hatajiunga tena na bodi."

Mmiliki huyo wa Tesla atasalia kuwa mwanahisa mkubwa zaidi wa Twitter na kampuni atakuwa wazi kupokea maoni yake, aliongeza.

Zaidi ya saa moja baada ya tangazo la Bw Agrawal, Bw Musk alitweet emoji moja. Tweet hiyo imefutwa.

Mwishoni mwa juma, Bw Musk alipendekeza mabadiliko kwenye huduma ya usajili ya Twitter Blue premium, ikiwa ni pamoja na kupunguza bei yake, kupiga marufuku utangazaji na kutoa fursa ya kulipa kupitia cryptocurrency dogecoin.

Bw Musk pia aliwauliza wafuasi wake zaidi ya milioni 81 ikiwa Twitter "inakufa" na ikiwa makao yake makuu yanapaswa kugeuzwa makazi ya watu wasio na makazi.

Pia alifanya kura ya maoni akiuliza ikiwa herufi "w" inapaswa kuondolewa kwenye Twitter, na chaguzi pekee zikiwa "ndio" na "bila shaka".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live