Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elon Musk: Wafanyabiashara na Serikali watalipia ada ili kutumia Twitter

Elon Mask111.png Elon Musk

Wed, 4 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara na Serikali wanaotumia mtandqo wa Twitter huenda wakahitajika kulipa "ada kidogo" ili kusalia kwenye mtandao huo wa kijamii.

Hii ni baada ya bodi ya Twitter kukubali ofa ya kuchukua dola bilioni 44 (£34.5bn) kumuuzia mtandao huo bilionea namba moja duniani, Elon Musk.

Hata hivyo, Musk amesema mtandao huo daima utakuwa wa bure kwa "watumiaji wa kawaida lakini kwa wafanyabiashara na Serikali watatakiwa kulipia ada kidogo ili waweze kutumia Twitter," alisema Elon kupitia akaunti yake ya Twitter jana Jumanne.

Mmiliki huyo wa makampuni ua Tesla na SpaceX alisisitiza kuwa account za watumiaji wa Twitter hazitabadilika kama baadhi ya maneno ambavyo yamekuwa yakizushwa mitandaoni.

Hapo awali alisema anataka "kufanya Twitter kuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa kwa kuboresha muonekano wake na kuongeza vipengele vipya kwa watumiaji wake".

Tangu kukubali kununua Twitter, Musk amesema alitaka kufanya maboresho ili kusaidia kuongeza mvuto wa kile anachoeleza kuwa jukwaa "maalumu".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live