Kwenye mahojiano yake na Mathias Döpfner ambaye ni mkurugenzi mkuu wa makampuni ya ''Axel Springer SE'' Bilionea namba moja Duniani Elon Musk amefunguka kwa mara ya kwanza kwa kudai kwamba kwa mtazamo wake anadhani kuwa Vladimir Putin ambaye ni Rais wa urusi ni tajiri zaidi yake.
Mathias: Kuwa na utajiri zaidi ya Dola Bilion 230 unatajwa kuwa tajiri namba moja Duniani
Elon Musk: Nadhani Putin anautajiri mkubwa zaidi yangu,
Mathias: Unaamini hivyo?
Elon Musk: Sawa, Ninachojaribu kumaanisha siwezi kuvamia nchi na vilivyomo, Nina amini kwenye msemo wa zamani wa Crassus unaosema "Bado huwaja tajiri mpaka uwe na uwezo wa kumiliki jeshi"
Huyu Marcus Crassus ni moja kati ya viongozi wa Romani aliyehesabiwa kuwa na utajiri mkubwa kwa wakati huo, aliwahi kusema utahesabiwa kuwa tajiri pale tu ambapo kipato chako kitaweza kumiliki jeshi.
Na Jeshi alilokuwa akilimaanisha Marcus Crassus, siyo hilo la Harmonize hili ni jeshi haswa lenye kuanzia watu 5000 - 6000 sasa vuta picha idadi kubwa hivi ya watu unawalipa kwa pesa ya mfukoni mwaka.
Na kwa ukumbusho zaidi upande wa kiimani walipokuwa wanahubiri kulikuwako na idadi kubwa ya watu kushuhudiwa inasemwa watu elfu tano ndiyo idadi ya kusanyiko lile, Filipo akajibu, “Wote tunapaswa kufanya kazi kwa mwezi mmoja ili kununua mikate ya kutosha na kumpa kila mmoja aliyepo angalau kipande kidogo.”
Kutokea hapo unaweza kupata mwanga wa namna gani, watu elfu tano ni wengi mnoo lakini kwa kiasi cha pesa alicho nacho Elon Musk hawezi kumiliki jeshi?