Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ellon Musk kulipa kodi zaidi ya Tsh. Trilioni 25 mwaka huu

Dhjkj Ellon Musk kulipa kodi zaidi ya Tsh. Trilioni 25

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CEO wa kampuni ya kutengeneza magari ya umeme ya Tesla Inc Elon Musk amesema kupitia Twitter kwamba atalipa zaidi ya dola bilioni 11 (Tsh. Trilioni 25) za ushuru mwaka huu.

Mapema wiki hii, Seneta wa chama cha Democratic nchini Marekani, Elizabeth Warren kupitia Twitter aliandika kwamba Musk anapaswa kulipa ushuru na kuacha "kupakia kila mtu bila malipo" baada ya jarida la Time kumtaja kama "mtu bora wa mwaka".

Musk alijibu kwa kusema kwamba "atalipa ushuru zaidi kuliko Mmarekani yeyote katika historia mwaka huu".

Musk ndiye mtu tajiri zaidi duniani na kampuni yake ya Tesla inatajwa kuwa na thamani ya takriban $1 trilioni. Katika wiki chache zilizopita, Musk ameuza hisa za Tesla zenye thamani ya karibu dola bilioni 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live