Vijana na Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Msingi wametakiwa kujengwa katika masuala ya fedha ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi kwa kujiletea maendeleo.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Chama cha Wahasibu Wanawake (TAWCO ) Tumaini Lawrence wakati wa maadhimisho ya Wiki Fedha Duniani ambayo imeratibiwa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampas ya Dar es Salaam ,amesema kuwa suala la fedha linatakiwa kila mmoja ajue kwani asilimia 54 ya watu wanaopata msongo wa mawazo ni kutokana na fedha.
Amesema wiki ya Fedha Duniani tangu kuanza kuadhimishwa lengo lake lilikuwa ni watu kupewa uelewa wa fedha kwani wakijengwa wanakuwa watu makini na hata wakiwa kazini hawawezi kuwa wala rushwa.
"Watu kuwa na uelewa wa fedha katika kufanya mipango tangu akiwa na umri mdogo ni vigumu katika umri mkubwa kuweza kupangilia fedha kwani ndio anakuwa amezipata kwa mara ya kwanza hivyo lazima jamii ielemishwe masuala ya fedha "amesema Tumaini
Tumaini amesema Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Tawi la Dar es Salaam wameona mbalimbali katika kushirikisha wanafunzi wa Vyuo , Shule za Sekondari,Msingi pamoja na wadau wa Kilimo na Mifugo kwa kuamini kuwa ndio watu kupata elimu hiyo katika kujijenga kifikra katika masuala ya Fedha.
Mratibu wa Wiki ya Fedha wa IAA Vaileth Maira amesema katika wiki hiyo itakuwa yenye mafakio ya kuwajenge a uwezo wadau pamoja na kuwa na mjadala wa masuala ya fedha.