Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elimisheni watu watu umuhimu wa kodi

Tax Tax Ushuruuuu Elimisheni watu watu umuhimu wa kodi

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waandishi wa habari wa mitandao ya Kijamii wametakiwa kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti halali yenye thamani halisi ya huduma waliyoipata.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, wizara ya Fedha Benny Mwaipaja amesema hayo leo Oktoba 23, 2023 wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika mkoani Morogoro.

“Mitandao ya Kijamii imekuwa nyenzo kubwa ya kuifikia jamii kwa haraka na kwa ukubwa, hivyo niwaombe mtumie fursa hiyo kuielimisha jamii umuhimu wa kudai risiti yenye thamani halali ya huduma uliyoipata". Amesema Mwaipaja

Amewataka wanamitandao hao kuisaidia Serikali kuielimisha jamii kuhusu ajenda ya maendeleo ya Taifa na miradi inayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya maslahi ya Watanzania ikiwemo miradi ya kimkakati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live