Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EWURA yatangaza uhaba mafuta ya taa

Mafuta Ya Taa.png EWURA yatangaza uhaba mafuta ya taa

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bei ya mafuta ya taa imeongezeka kwa wastani wa Sh39 kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Mtwara na Tanga mwezi Machi ikilinganishwa na Februari 2023, huku uhaba wa bidhaa hiyo ukitawala.

Katika taarifa ya bei mpya za mafuta iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Dk James Mwainyekule imeonyesha kuisha kwa bidhaa hiyo katika matanki yaliyopo Tanga.

"Kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye matanki ya kuhifadhia yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam," imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia imeonyesha katika bandari tatu za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga zinazopokea mafuta ni mbili pekee (Tanga na Dar es Salaam) ndio zenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya taa.

Kutokana na kuisha kwa mafuta ya Tanga katika Bandari ya Tanga, hivyo nchi nzima kwa sasa inategemea mafuta ya taa kutoka Bandari ya Dar es Salaam huku athari ya kuongezeka kwa bei ya mafuta hayo imeongezeka.

"Bei ya mafuta ya taa mkoani Tanga imeongezeka kutoka Sh3,107 Februari Hadi Sh3,144 Machi, huku Mtwara ikiongezeka kutoka Sh3,134 hadi Sh3,170 mwezi huu," imesema taarifa hiyo.

Wakati mafuta ya taa yakipatikana katika bandari moja pekee, takwimu za ripoti ya mwisho wa mwaka ya Ewura inaonyesha kupungua kwa uagizaji wa mafuta ya taa kwa asilimia 28 mwaka 2020/2021 ikilinganishwa na mwaka 2019/2020.

"Mwaka 2019/2020 lita 38.47 milioni yaliingia nchini kabla ya kupungua Hadi lita 27.86 milioni mwaka 2020/2021," ripoti ya Ewura ya Mwaka 2021 imeonyesha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live