Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EWURA kuratibu ujenzi vituo vya mafuta vijijini

Mnj Ewura kuratibu ujenzi vituo vya mafuta vijijini

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na maji (Ewura) imesema inakuja na mpango mkakati wa ujenzi wa vituo vya mafuta vya gharama nafuu maeneo ya vijijini nchini ili kukabiliana na uuzwaji holela wa mafuta yasiyo na ubora kwenye chupa.

Meneja wa Mawasiliano na uhusiano Ewura Makao Makuu, Titus Kaguo amesema leo Oktoba 9, 2021 mkoani Mbeya kwenye warsha ya kuwajengea uwezo wandishi wa habari mikoa ya Nyanda za Juu Kusini namna ya kuandika habari zinazohusina na Mamlaka hiyo.

"Katika udhibiti wa nishati ya mafuta nchini, Ewura tunahitaji kuondo biashara za uuzwaji holela wa mafuta kwenye chupa unaofanywa maeneo ya vijijini kwa kuwezesha kampuni zenye uwezo kujenga vituo vya gharama nafuu ili kufikisha huduma bora," amesema.

Amesema lengo ni kuboresha upatikanaji wa huduma hizo si mijini peke bali hata viijijini sambamba na kuendelea kukabiliana na udhibiti wa nishati ya maji,gesi na mafuta kwa kuhakikisha vinakuwa na ubora kwa matumizi ya wateja na wananchi kwa ujumla"amesema.

Aidha kwa upande mwingine amewataka wamiliki wa magari ya umma na binafsi kutoa taarifa za wafanyabishara wa vituo vya mafuta wanaotumia ujanja kuwaibia kwa kuchakachua pampu za kujazia mafuta ambao umeibuka katika baadhi ya maeneo nchini.

"Kuna mchezo ambao unaweka mafuta lita 10, lakini kwa namna wanavyofanya kwenye pampu ukapata lita 5 sasa ili kuwabaini naomba muwe mnashuka na kushuhudia mashine zinavyosima sambamba na kuchukua risiti ambazo zitatusaidia ushahidi kama Mamlaka yenye dhamana," amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Ewura, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Karim Ally amesema kuwa ili kudhibiti mchezo huo kuna kila sababu wananchi kusaidiana na Ewura kutoa taarifa zinazohusiana na Sekta wanazosimamia.

Chanzo: mwananchidigital