Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EWURA kufungia vituo 5 vya mafuta

EWURA EWURA kufungia vituo 5 vya mafuta

Fri, 26 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kusudio lake la kuvifungia vituo vitano vya mafuta, vikubwa vikiwa viwili.

Vilevile, vipo vilivyopewa onyo na kimoja kikipewa adhabu ya kulipa faini ya Sh. milioni sita kutokana na kitendo chake cha kuuza mafuta juu ya bei elekezi na kutotoa risiti kwa wateja.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo, alisema mamlaka hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kutoa muda wa saa 48 za kujitetea kwa vituo hivyo ambapo baadhi vilifanya hivyo na vingine havikutoa maelezo yoyote.

Alivitaja vituo ambavyo vipo kwenye kusudio la kufutiwa leseni ni mteja wa jumla aliyeko Kigamboni jijini Dar es Salaam ambaye ni Mansoor Industry.

Vingine ni kituo cha mafuta cha BO5 Ways Petrol cha Bagamoyo kinachouza kwa rejareja, Mexon Energy Ltd cha Makambako, Mexon Energy Ltd cha Njombe na Olimpic.

Kaguo alitaja vingine ambavyo vimepewa onyo ni Oryx, Star Oil Tanzania Ltd ambaye amechunguzwa na amejitetea, lakini bado wanaendelea kumchunguza na asipoangalia naye atafutiwa leseni.

“Vingine ni Come Oil ambaye alijitetea kuwa hakuwa na mafuta kwa sababu yalishikiliwa, hivyo amesamehewa.

“Kituo kingine ni Mtweve Oil cha Chunya ambacho kilikutwa na kosa mara mbili la kuuza mafuta bei ya juu ya kikomo badala ya Sh. 1,637 walikuwa wakiuza Sh. 1,985, hivyo watatakiwa kulipa faini Sh. milioni sita na kosa jingine ni la kutotoa risiti,” alisema.

Hata hivyo, alisema upo utaratibu wa kukata rufani, lakini wanaamini hawatashinda.

Kaguo alisema bodi ya EWURA inakusudia kufanya marekebisho ya leseni za uuzaji wa mafuta na kwamba kabla ya mtu kupatiwa atatakiwa aonyeshe ana vituo vingapi ili kuondoa tatizo la mafuta hasa kwa wateja wa rejareja.

Pia, alikiri kuwapo kwa dalili za baadhi ya watu kuficha mafuta ili kushinikiza bei ipande.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live