Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EWURA: Marufuku kuuza mafuta bila bango la bei

Mafuta Mjadala EWURA: Marufuku kuuza mafuta bila bango la bei

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imevitaka vituo vyote vinavyouza mafuta, kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari imesema, ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei yanayoonekana vizuri kwa wateja.

EWURA imesema adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live