Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU, Tanzania kuboresha uwekezaji

Uchumi Kupanda EU, Tanzania kuboresha uwekezaji

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya masuala ya kiuchumi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) Karina Dzialowska, amesema kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Hayo ameyabainisha alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida na kujadiliana kuhusu namna wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kuibua mikakati mbalimbali inayolenga kuongeza uwekezaji nchini.

Aidha Karina alibainisha uwepo wa fursa ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uwekezaji katika miradi rafiki kwa mazingira (Green investment) ambayo itatokana na fedha zinazopatikana kupitia masoko ya mitaji kwa amana mahsusi kwa ajili ya miradi rafiki kwa mazingira (Green Bonds).

Vilevile, katika kikao hicho viongozi hao wamezungumzia utekelezaji wa mpango wa maboresho ya mazingira ya Biashara na Uwekezaji (BLUE PRINT) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Business Environment Growth Innovation (BEGIN)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live