Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU, Namibia kushiriki kongamano la biashara nchini

Eu Biashara Biashara (600 X 362) EU, Namibia kushiriki kongamano la biashara nchini

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Ulaya (EU) na Namibia wanakuja kwa mara ya kwanza na jukwaa la biashara, likilenga kipekee haidrojeni ya kijani na malighafi muhimu.

Jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 24 mwaka huu jijini Brussels, Ubelgiji, kwa mujibu wa Goasia Lachut, Mkuu wa Shughuli za Ubelgiji nchini Namibia.

Jukwaa hilo limeandaliwa kwa pamoja na Bodi ya Uendelezaji na Ukuzaji Biashara ya Namibia (NIPDB) na EU. Lachut aliwaambia wana habari jijini hapa kwamba malengo hasa ya jukwaa hilo ni kuiunga mkoni Namibia katika jitihada zake za kuvutia uwekezaji kutoka Ulaya, na kukuza ushirikiano wao.

“Jukwaa hili limekuja muda mwafaka, kwani linajengwa kwenye maridhiano yaliyosainiwa baina ya Rais Hage Geingob na Rais wa Kamisheni ya EU, Ursula von der Leyen mwaka 2022, wakianzisha usharika wa kimkakati kati yao. Jukwaa hilo litaendeshwa chini ya kaulimbiu; ‘Kuhamasisha uwekezaji wa ubora na kuongeza thamani kwa ukuaji wa kijani katika ushirikiano wa EU-Namibia’, kwa kuzingatia hidrojeni ya kijani na minyororo ya thamani ya malighafi muhimu.

Jukwaa la Biashara la EU-Namibia litaanza kwa hafla ya ufunguzi, ikimshirikisha Rais Geingob, na viongozi wengine waandamizi kutoka sekta ya umma na sekta binafsi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live