Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EACO yajidhatiti kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki

Eaco Pic Data EACO yajidhatiti kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati-tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) imejidhatiti kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki. Mtendaji Mkuu wa EACO, Dk Ally Simba alisema wamedhamiria kuhakikisha wanakuza mahusiano katika mashirika katika taasisi wanachama ili kuwepo usimamizi mzuri wa huduma za mawasiliano. “Tumedhamiria kuhakikisha mashirikiano baina ya taasisi zetu yanaimarika ili tukuze usimamizi thabiti wa huduma za mawasiliano katika nchi wanachama” alisema Simba. EACO imeweka mkakati huo kwenye kikao kazi cha kamati hiyo kilichoketi, Bububu, Zanzibar mapema wiki hii. Kikao kazi cha Kamati hiyo inayoundwa na Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Usimamizi wa mawasiliano za Afrika Mashariki kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya, Ezra Chiloba; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usimamizi wa Mawasiliano Burundi, Samuel Muhizi; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani Kusini, Napoleon Adok Gai; Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano -Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo; Mtendaji Mkuu wa EACO Mtanzania Dk. Ally Simba; na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Rwanda, Deo Muvunyi.

Kamati-tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) imejidhatiti kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki. Mtendaji Mkuu wa EACO, Dk Ally Simba alisema wamedhamiria kuhakikisha wanakuza mahusiano katika mashirika katika taasisi wanachama ili kuwepo usimamizi mzuri wa huduma za mawasiliano. “Tumedhamiria kuhakikisha mashirikiano baina ya taasisi zetu yanaimarika ili tukuze usimamizi thabiti wa huduma za mawasiliano katika nchi wanachama” alisema Simba. EACO imeweka mkakati huo kwenye kikao kazi cha kamati hiyo kilichoketi, Bububu, Zanzibar mapema wiki hii. Kikao kazi cha Kamati hiyo inayoundwa na Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Usimamizi wa mawasiliano za Afrika Mashariki kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya, Ezra Chiloba; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usimamizi wa Mawasiliano Burundi, Samuel Muhizi; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani Kusini, Napoleon Adok Gai; Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano -Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo; Mtendaji Mkuu wa EACO Mtanzania Dk. Ally Simba; na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Rwanda, Deo Muvunyi. EACO ilianzishwa mwaka 2012, kama muungano wa kikanda wenye sura ya kimataifa na kikanda ukilenga kuwaleta pamoja wasimamizi wa mawasiliano na wadau wa sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki kwa shabaha ya kuboresha usimamizi na utoaji huduma za mawasiliano kwa wananchi wa Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live