Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAC: Mchakato wa kupata noti ya pamoja haujakamilika

Eac Sudan.jpeg EAC: Mchakato wa kupata noti ya pamoja haujakamilika

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetaka kupuuzwa kwa taarifa iliyosambaa mitandaoni ikidai kuwa Jumuiya hiyo imetambulisha noti mpya ya pamoja itakayotumika katika nchi wanachama iitwayo SHEAFRA.

EAC imesema mchakato wa kupata noti ya pamoja bado unaendelea hivyo taarifa kuwa kuna noti ya pamoja ni uzushi.

Taarifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuja huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba naye akikanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa X.

"Hizi taarifa si za kweli, taarifa na vigezo vya kiuchumi na kitaasisi vya kufikiwa kwa Umoja wa Fedha (Monetary Union)/Sarafu Moja (Single Currency) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado kukamilika, mapendekezo ni kufika hatua hiyo mwaka 2031," Ilisema taarifa hiyo ya Waziri Makamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live