Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EABC yashawishi uboreshaji miundombinu mpakani

45860878767a4d0170d738aeabc8237e EABC yashawishi uboreshaji miundombinu mpakani

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BARAZA la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limetoa wito kwa wadau wa Jumuiya hiyo kuweka kipaumbele uboreshwaji wa miundombinu katika mipaka ili kuwezesha mtiririko wa bidhaa na uhuru wa wananchi kuvuka mipaka kwa lengo la biashara.

Miundombinu mibovu inaendelea kuwa kikwazo kikubwa cha biashara Afrika Mashariki.

Hayo yalibainika baada ya ziara iliyofanywa katika Kituo cha Mpakani cha Busia One-Stop (OSBP) na EABC ilibaini kituo hicho kinafanya kazi kwa ufanisi. Karibu malori 1,000 yaliyo na bidhaa hupitia mpaka siku za wiki na idadi iliongezeka hadi malori 2,000 mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, Dk Peter Mathuki alipendekeza kuboreshwa kwa miundombinu katika Busia One-Stop Border Post kupitia ujenzi wa barabara ya njia nne ili kupunguza foleni.

“Njia ya kwanza inapaswa kusafirisha shehena ya jumla, njia ya pili kutumiwa na abiria ya tatu inaweza kuwa ya mazao safi na ya nne kwa bidhaa zenye hatari,” alisistiza Dk Mathuki.

Kadhalika Dk Mathuki pia alisisitiza hitaji la nafasi za maegesho kujengwa kwa malori ya mizigo karibu na Busia OSBP.

Alisema kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), eneo la Afrika Mashariki linakadiriwa kupata nafuu hadi asilimia 3.7 katika hali ya msingi na asilimia 2.8 katika hali mbaya zaidi mwaka huu, kwa kudhani kuwa COVID-19 itapatikana katika kipindi kifupi na kwa muda wa kati.

Chanzo: habarileo.co.tz