Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Drone utafiti wa madini yarushwa Mirerani...

Faa Drones 660x400 Drone utafiti wa madini yarushwa Mirerani...

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inashirikiana na Kampuni za Tukutech Company Ltd kutoka Tanzania, Zanifi Enterprise Ltd kutoka Zambia na Radai OY kutoka nchini Finland kurusha ndege nyuki (drone) angani kwa ajili ya kufanya majaribio ya tafiti za miamba na madini katika eneo la Mirerani, kwa kutumia teknolojia ya High Resolution Airborne Geophysical Survey.

Akizunguza katika semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jana Februari 13, 2024 jijini Dodoma, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema dhamira ya Serikali ni kuona Tanzania inafanyiwa utafiti wa kina kuhusu madini na wizara hiyo imekuja na ajenda ya Vision 2030.

Mavunde amesema ‘Madini ni maisha na mtajiri’ kwa kufanya tafiti kwa njia ya jiofizikia angalau utafanyika kwa asilimia 50 ifikapo 2030, ambapo kwa sasa ni asilimia 16 pekee ambayo imefanyiwa utafiti huo.

"GST ni moyo wa sekta ya madini, uwepo wa taarifa sahihi za kijiolojia ya miamba na madini ndiyo imebeba dhana ya utajiri wa Tanzania, hivyo niwaombe wajumbe wa kamati hii tuisaidie GST kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu," amesema Mavunde.

Imeelezwa kuwa, awamu ya kwanza ya majaribio ya tafiti za miamba na madini ilifanyika mwaka jana (2023) katika mikoa ya Dodoma, Shinyanga na Geita ambapo awamu ya pili ya utafiti huo unafanyika katika mikoa ya Lindi, Mtwara na eneo la Mirerani mkoani Manyara.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Dk Suleiman Serera ameipongeza Wizara ya Madini kupitia GST kwa kutekeleza kwa vitendo dhana ya Vision 2030, ikiwa ni pamoja na kuratibu shughuli ya utafiti ndani na nje ya ukuta wa Magufuli, Mirerani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live