Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dreamliner yatua Mwanza na kikosi cha Simba

12392 Pic+dream TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Baada ya kukosekana angani kwa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 14 hadi 16, 2018  ndege ya Boeing 787-7 Dreamliner  imeanza tena kukata anga na tayari imetua katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

MCL Digital  iliyopiga kambi uwanjani hapo tangu asubuhi imeshuhudia ndege hiyo ikitua saa 3:48 asubuhi leo Agosti 17, 2018.

Miongoni mwa abiria waliokuja na ndege hiyo ni pamoja na kikosi cha timu ya soka ya Simba Sports Club ambayo kesho inacheza mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Mtibwa Sugar kufungua pazia ya ligi kuu ya Tanzania.

Akizungumza na MCL Digital  kwa njia ya simu, Kaimu Meneja wa Uwanja wa ndege Mwanza, Julius Msofee amesema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 262 tayari imeruka kuendelea na safari kwa mujibu wa ratiba yake.

“Dreamliner imetua salama na tayari imeruka kuendelea na safari kwa mujibu wa ratiba. Miongoni mwa abiria waliokuja nayo ni wachezaji na viongozi wa timu ya Simba,” amesema Kaimu Msofee.

Ndege hiyo iliyozindua safari zake Julai 29, 2018 ilisitisha safari zake kati ya Dar es Salaam – Kilimanjaro – Mwanza tangu Agosti 14 kwa kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege nchini (ATCL), Ladislaus Matindi kuwa ni matakwa ya kiufundi ikiwamo kuangalia marekebisho ya suala la WiFi inayotakiwa kufanya kazi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz