Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma yatumia madaftari kuongeza uzalishaji wa chakula

12752 DODOMA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 20 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Uwapo wa madaftari matatu kwa ajili ya takwimu za wakulima wa mazao mbalimbali ya chakula katika Jiji la Dodoma umeongeza uzalishaji wa chakula kutoka tani 462,148 mwaka 2016/17 hadi tani 803,710 mwaka 2017/18.

Daftari la kwanza linaonyesha jina la mwananchi na eka alizolima na upande wa kulia wa daftari hilo linaonyesha sehemu ambayo mwenyekiti wa kijiji anaweka sahihi kuthibitisha kila mwananchi amelima eka kuanzia mbili.

Daftari la pili, linatakuwa linakaa kwa mwenyekiti wa kijiji kwa ajili ya ofisa ugani ili akienda kufanya ukaguzi wa miradi ya wananchi anatakiwa kuweka sahihi na kuonyesha idadi ya miradi aliyoikagua.

Daftari la tatu ni kwa ajili ya viongozi kama vile mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa pindi akienda kufanya ukaguzi anatakiwa kuweka sahihi ishara ya kuonyesha kile alichokiona kimesimamiwa nyema na viongozi wa ngazi ya chini.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 19, 2018 wakati wa kuwasilisha taarifa  ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha miaka miwili na nusu katika kikao cha halmashauri kuu mkoa wa Dodoma, mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk, Binirithi Mahenge amesema kuwapo kwa madaftari hayo kumeongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao ya chakula.

“Na hii imesaidia kumfanya kila mtu awe anafanya kazi katika nafasi yake, pia imesaidia kupata takwimu kamili kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya na hata mkoa kwa sababu tunajua ni hekari ngapi za mihogo zimelimwa na uzalishaji wake ni kiasi gani,” amesema Dk, Mahenge.

Dk Mahenge amesema madaftari hayo yatausaidia Mkoa wa Dodoma na wakazi wake kuondoa njaa katika maeneo mbalimbali.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz