Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Mwinyi aikubali Serikali JMT, bodi TAEC ujenzi maabara ya Atomu

331750111 6106898586063975 2176358094834458563 N Dkt. Mwinyi aikubali Serikali JMT, bodi TAEC ujenzi maabara ya Atomu

Thu, 16 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bodi na Menejimenti ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).

Rais Mwinyi ametoa pongezi kwa mamlaka hizo za Serikali kwakuona umuhimu wa ujenzi wa Ofisi na maabara inayolenga kuimarisha huduma za Nguvu za Atomu Zanzibar.

Amesema, Uwekezaji huu utaimarisha udhibiti wa matumizi salama ya mionzi pamoja na kuimarisha utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Pongezi hizo zimetolewa na Dkt. Mwinyi wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania(TAEC), zilizopo eneo la Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live