Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Kikwete atoa neno maonesho Viwanda na Biashara

WhatsApp Image 2022 10 08 At 18.16.32 1080x640.jpeg Dkt. Kikwete atoa neno maonesho Viwanda na Biashara

Mon, 10 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefungua maonesho ya tatu ya Viwanda na Biashara Mkoa wa Pwani.

Mara baada ya kufungua maonesho hayo, Dkt. Kikwete alitembelea banda la Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF), ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa jamii, Masha Mshomba alimpa maelezo juu ya huduma zitolewazo na NSSF.

NSSF, inashiriki Maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kueleza fursa mbalimbali za Uwekezaji, kutatua kero za wanachama na kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Maonesho hayo, yanaendelea katika stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani, na yatafikia kilele chake Oktoba 10, 2022.

Chanzo: Dar24