Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt.Kijaji: Changamkieni fursa AGOA

Dkt Kijaji Awataka Wafanyabiashara Dodoma Kuchangamkia Fursa Dkt.Kijaji: Changamkieni fursa AGOA

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu kijaji amewataka Wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa ya Sheria ya ukuaji wa fursa Afrika(AGOA) ili kupata masoko nje ya nchi hususani nchini Marekani.

Dkt. KIjaji amebainisha hayo katika kikao cha pamoja na wadau wa mpango wa AGOA kilichofanyika mkoani Dar es Salaam na kuwakutanisha Wafanyabiashara na Serikali.

Amewataka Wafanyabiashara kwenda pamoja na fursa hiyo ili kukimbia kwa pamoja katika soko la bidhaa duniani kwa kuzingatia ubora wa bidhaa pamoja na uzalishaji wa bidhaa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda katika ufanyaji wa shughuli zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live