Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Olomi ataka kubadili maandishi kwenye uhalisi

20903 Mtazamo+pic TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Tanzania inahitaji mjadala mpana kuhusu dhana ya kubadili mtizamo ili kukamilisha safari ya kuwa nchi ya viwanda.

Akizungumza leo Oktoba 4,2018  kwenye Jukwa la Fikra la Mwananchi linalolenga kujadili fursa, changamoto na ufumbuzi kuelekea uchumi wa viwanda ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya utawala na ujasiriamali, Dk Donath Olomi amesema mitizamo  ni kikwazo kwa Watanzania wengi.

Dk Olomi amesema tatizo lipo kwenye mfumo wa elimu, hakuna mipango ya muda mrefu kubadili mtizamo kuelekea kwenye mfumo wa Tanzania ya viwanda.

Amefafanua kuwa inatakiwa kuwe na kampeni maalumu kama ilivyokuwa kwenye masuala ya jinsia, Ukimwi na malezi.

"Wengi wanaamini kwenye vyeti, wanashikilia wanafunzi wakipeleka vyuo vikuu wanapewa vyeti na kuachiwa wakiambiwa wameshawachoka," amesema na Dk Olomi na kuongeza:

"Hiyo ni sawa na kumfundisha mamba kuogelea baada ya muda unampa cheti na kusema ameelewa kuogelea, ilhali angekaa kwenye maji angefanya kazi nzuri sana."

Dk Olomi amesema nchi ipo kwenye hatua ndogo ya kukuza ujasiriamali, kwa kiasi kikubwa inategemewa Shirika la Kuhudumia Wiwanda Vidogovidogo (Sido) ambayo inatumia sheria ya mwaka 70.

Ameeleza uhitaji wa taasisi za kuangalia wajasirimali wanaochipukia na kuwasogeza mbele, inahitaji kuwekeza nguvu kubwa ili wavuke.

"Taasisi zinazolilinda hili eneo ni chache sana, kama Serikali bado siyo kipaumbele chake," amesema.

Amesema vyuo vya ufundi vipanuliwe vijana wapewe elimu waajiriwe, wajiajiri na teknolojia inayotumika iboreshwe kupata matokeo chanya.

"Teknolojia unayotumia kwenye kilimo bado ni duni ndiyo maana wakulima wanashindwa kupata wanachostahili," amesema.

Dk Olomi amesema hakuna haja ya kuendelea kupanga na kuzungumza, kuweka mkakati kwenye maandishi badala yake waende kwenye uhalisia.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz