Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mwinyi asisitiza matumizi ya EFD

6b8824a32a63cbe03425e77de5fc8edd Dk Mwinyi asisitiza matumizi ya EFD

Tue, 1 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewataka wafanyabiashara wa Zanzibar watumie mashine za kielektroniki za ukusanyaji wa mapato (EFD) ili kurahisha ukusanyaji mapato ya serikali.

Akizungumza kupitia utaratibu wake wa kuzungumza na vyombo vya habari kila mwisho wa mwezi, Dk Mwinyi alisema utaratibu wa kutumia mashine hizo ni wa lazima kwa kuwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria.

Alisema ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuhakikisha analipa ushuru kupitia mashine hizo na kuachana na utoaji wa risiti za mkono alizosema matumizi yake yamejawa udanganyifu.

Alisema wafanyabiashara wakiandika risiti kwa mkono ni tatizo kwa kuwa haioneshi nani katumia bidhaa gani na kodi ya serikali ni kiasi gani.

“Hapa kuna upinzani kwa sababu bado kuna wafanyabiashara wengi hawataki fedha hii iende serikalini, wanataka bado waichukue wao, tunasema hii ni sheria haina mjadala... Lazima watu walipe VAT kwa matumizi ya bidhaa zote wanatumia,” alisema Dk Mwinyi.

Alisema pamoja na suala hilo kupata changamoto ya upinzani kutoka kwa wafanyabiashara hao, ni lazima sheria itekelezwe kwani halitokuwa la kwanza kufanywa na Zanzibar pekaa bali Tanzania Bara na Dunia nzima inatumia mfumo huo ambao lengo lake ni kuhakikisha mapato ya uhakika yanapatikana

Mbali na hilo, Dk Mwinyi alisema malalamiko kuhusu gharama kubwa kwa ajili ya ununuzi wa mashine hizo kiasi cha Sh 400,000 hususani kwa wafanyabiashara wadogo lisiwe hoja kwa kwani litatafutiwa utaratibu kwa wafanyabiashara hao kulipa kwa awamu hadi watakapomaliza gharama ya kifaa hicho.

“Hoteli zote karibu ya 600 zilizopo hapa Zanzibar, sidhani kama kuna hoteli inashindwa kulipa, tatizo linaweza kuwa kwa wafanyabishara wadogo wa madukani… Tunasema tusigombane kwa hilo, tatafuta utaratibu wa watu walipe kwa awamu, lakini Sh 400,000 lazima ilipwe kwa sababu kifaa kile hakitolewi bure. Ukitumia kifaa hiki baada ya muda mfupi sisi tutaipata hiyo Sh 400,000, nawataka ZRB itengeneze utaratibu wa kuwalipisha kwa awamu,” alisema Dk Mwinyi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live