Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mwinyi ainadi Tanzania SADCOPAC

Dkt. Hussein Ali Mwinyi  . Dk Mwinyi ainadi Tanzania SADCOPAC

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema serikali zote mbili (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar) zinafanya jitihada kubwa kukabiliana na vitendo vya rushwa na kuhimiza uwajibikaji ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 pamoja na mipango mingine ya maendeleo.

Rais Mwinyi amesema hayo leo Aprili 17, 2024 alipofungua rasmi Mkutano wa mafunzo kwa wajumbe na wataalam wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ya Hesabu za Mashirika ya Umma (SADCOPAC) katika kupambana na rushwa, kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa maliasili unaofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar

Aidha, Dk Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar inasimamia masharti na maelekezo ya miongozo ya kamati ya SADCOPAC kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatekeleza kikamilifu makubaliano yaliyoafikiwa baina ya nchi wanachama.

Pia, Dk Mwinyi amesema Zanzibar imeanzisha utaratibu wa kusomwa hadharani taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kujadiliwa kwa uwazi na kina katika Baraza la Wawakilishi.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi ametoa wito kwa nchi wanachama wa JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuziimarisha taasisi zinazohusika na utawala bora kwa kuzipatia wataalam zaidi wa fani mbalimbali ili ziwe na upeo mkubwa zaidi wa kufanya uchunguzi kwa mujibu wa majukumu yao. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live