Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk.Mwinyi: Mfumo wa manunuzi mtandao mwarobaini wa urasimu

Mwinyi MShaharaaa (600 X 378) Mfumo wa manunuzi mtandao mwarobaini wa urasimu

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dk Mwinyi ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 25, 2022 wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao E-procurement Zanzibar ulioshirikikisha Wakala wa Serikali Mtandao e-Government, Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma na Oman Data Park katika hoteli ya Verde Mtoni.

“Hili sote ni mashahidi kuna wakati napokea malalamiko ya wazabuni na nikifuatilia zabuni zilizofanywa unashaangaa kuona yanayofanyika nadhani mwarobani wa hayo ni mfumo huu,” amesema

Amesema mfumo huo utaondoa changamoto sugu zilizokuwepo katika vitengo vya manunuzi na kuagiza kuwa mtendaji wa ngazi yoyote atakayeharibu au kudharau kwa makusudi kutumia mfumo huo na mifumo mengine iliyokuwa tayari atachukuliwa hatua.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleman amesema kuzinduliwa kwa mfumo huo ni kufungua ukurasa mpya kwani utaleta mafanikio makubwa na kuahidi mfumo huo hautochezewa.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya amesema watahakikisha mfumo huo hautakuwa wa hiari kwa taAsisi na mashirika ya Serikali bali ni jambo la lazima na watahakikisha wanausimamia kwa nguvu zote.

Advertisement Dk Saada amesema ofisi yake inakamilisha taratibu za kubadilisha Sheria ya manunuzi namba 11 ya mwaka 2011 ili kuona sheria hiyo inaendana na wakati wa sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E –Government), Said Seif Said amesema wamehakikisha mfumo huo kuwa na uwezo mkubwa lakini mafanikio yake itategemea jinsi watendaji katika taasisi hizo watakvyoupokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live