Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mwigulu apendekeza mabadiliko mfumo ununuzi wa umma

Mwiguluuuuu Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema itaachana na mfumo wa sasa wa Ununuzi wa Umma (Transactional Procurement) kutokana na kile kilichoelezwa kuwa umeshindwa kuleta tija.   Hiyo ni baada ya kile kilichoelezwa kuwa msingi wake mkubwa umekuwa ni ulinganishaji wa zabuni zilizofunguliwa badala ya bei za bidhaa na huduma ambazo zinajulikana.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Juni 14, 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.

Dk Mwigulu amesema mara nyingi bei zinazowekwa katika mfumo huo zimekuwa kubwa kuliko zile zilizopo sokoni kwa jumla na hata rejareja.

“Ingekuwa tunanunua kwa ajili ya nyumbani kwetu au kwa ajili ya kampuni zetu tusingekubali bei hizo. Napendekeza kuwa, ununuzi wa umma uwe wa kwa kuzingatia ukubwa wa ununuzi wa Serikali na sekta ya umma kwa ujumla,”

 “Pamoja na uwiano na mfanano wa bidhaa na huduma zinazotumika serikalini na sekta ya umma yaani synergies. Sasa Serikali ni moja, bidhaa zinafanana, hata ofisi zilizoko mkoa mmoja, ila inatokea kila mmoja anakuwa na bei zake licha ya bidhaa kufanana,” amesema Dk Mwigulu.

“Tutaendelea kuboresha Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (TANePS) ikiwemo kuweka ukomo wa bei za bidhaa na huduma zinazotumika serikalini ili kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali,”

Amesema kama Wizara itahakikisha bei zote za bidhaa na huduma zinazotumika sokoni kwa jumla na rejareja zinaingizwa kwenye mfumo wa TANePS na kuwa kikomo cha bei zitakazotumika Serikalini.

“Hii itasaidia kuhakikisha kwamba mfumo wa TANePS hauruhusu watoa huduma na wakandarasi au wauza bidhaa wanaotoa bei zilizo zaidi ya soko kupata zabuni (tender) kwenye sekta ya umma,” amesema Dk Mwigulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live