Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mahiga: Serikali haijafikia mwafaka kusaini mkataba wa EPA

43998 Pic+mahiga Dk Mahiga: Serikali haijafikia mwafaka kusaini mkataba wa EPA

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Augustine Mahiga, amesema Serikali haijafikia mwafaka wa kutia saini mkataba wa makubaliano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya (Epa).

Kauli ya Dk Mahiga inakuja ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya kufikia muda wa mwisho uliotolewa na wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki (EAC).

Akizungumza na Mwananchi jana Dk Mahiga alisema suala hilo ni lazima lifuate utaratibu kabla ya kufikia hatua ya kusainiwa.

Alisema Serikali bado ipo katika mazungumzo na EU kuhusiana na suala hilo kukubaliana juu ya mambo muhimu yaliyomo katika mkataba huo kabla ya kufanya uamuzi.

“Ni mapema mno kwa sasa kuweka wazi masuala muhimu yaliyo katika mkataba huo ambayo tunaendelea kujadiliana ili kufikia makubaliano,” alisema.

Aliongeza kuwa Serikali na EU ni lazima wafikie mwafaka kwa kupata majibu ya maswali yote ya Tanzania kuhusiana na mkataba huo, kisha jambo hilo litawasilishwa bungeni.

Alisisitiza kuwa licha ya makubaliano yoyote yatakayofikiwa kati ya Serikali na EU uamuzi wa mwisho utafanywa na Bunge kama kusaini au kutosaini.



Chanzo: mwananchi.co.tz