Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mabula azindua kitabu cha uendelezaji miji

Mabula Kitabu Miji Dk Mabula azindua kitabu cha uendelezaji miji

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amezindua kitabu kinachojulikana kwa jina la ‘Bulding the Just City in Tanzania: Essays on Urban Housing’ kilichoandaliwa na taasisi ya Friedrich-Ebert-Stiftng (FES).

Kitabu hicho ambacho ni mkusanyiko wa insha zenye maudhui yaliyobeba jumbe mbalimbali zinazotoa mchango katika kupanga na kuendeleza miji na mfumo wa utawala unavyoweza kuathiri upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu kwa wote na masharti au utaratibu wa upatikanaji ardhi ambayo ndiyo msingi wa upataikanaji wa nyumba.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho jijini Dodoma leo Machi 21, 2023 Waziri Mabula amewataka wadau wa sekta ya uendelezaji milki kusaidiana na serikali kuogeza kasi ya ukuzaji miji iliyosalama na iliyopangwa vyema.

Amesema wadau wa upangaji na upimaji wanakaribishwa ili kuongeza kasi ya upangaji na upimaji ardhi ili kuwezesha watanzania kupata ardhi iliyopangwa na kupimwa ili kuepusha ama kuondokana na ujenzi holela na hivyo kuwa na miji inayokuwa katika utaratibu uliopangwa.

“Nimegundua kuwa kuna mapendekezo ya kisera kwa serikali kuu, mamlaka za serikali za mitaana wadau wengine ambayo yote yanalenga kuchangia kuboresha upatikanaji wa nyumba za bei nafuu zinazotosheleza, zinazofaa na salama” amesema Dk Mabula.

Mstahiki meya jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alisema miji mingi uendelezaji wake unaenda tofauti na mipango kabambe kutokana na uwezo mdogo wa halmashauri katika kutekeleza mpango huo jambo alilolieleza kuwa linachangia ukuaji wa miji holela.

‘’Implementation ya master plan, kwa upande wangu naona halmashauri zina uwezo mdogo wa kusimamia, serikali kuu inatakiwa kuwa mdau mkubwa katika suala hili’’ alisema Profesa Mwamfupe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live