Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Kimei alia na soko la mpakani mwa Tanzania na Kenya

Kimei Kimei Kimei Dk Kimei alia na soko la mpakani mwa Tanzania na Kenya

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema imeshatenga eneo la ukubwa wa ekari 140 katika eneo la Lokolova kwa ajili ya kujenga soko la mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Hatua inayofuata kwa sasa ni kupata hati miliki ya eneo hilo na hatimaye kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya soko hilo.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumatatu Mei 30, 2022 na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ambaye amesema Serikali inajua umuhimu wa kujenga soko hilo.

Kigahe alikuwa akijibu swali la mbunge wa Vunjo, Dk Charles Kimei ambaye amehoji ni lini Serikali itaanza ujenzi wa soko la Kimataifa katika eneo la Lokolova mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Dk Kimei ametaka kujua pia ni lini Serikali itakuja na mkakati wa kuweka mapaa kwenye baadhi ya masoko ili kuwasaidia wanawake na vijana wanaonyeshewa na mvua wanapokuwa kwenye biashara zao.

Naibu Waziri amesema Serikali inatambua umuhimu wa kujenga miundombinu hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, hivyo akaagiza halmashauri husika kutenga fedha kwa ajili ya kuanza kufanya ukarabati wa masoko hayo.

Advertisement Hata hivyo Kigahe amesema mara baada ya mkutano wa Bunge kuisha atakwenda kuangalia eneo hilo na kuona namna anavyoweza kuongeza nguvu ya msukumo ili kuharakisha ujenzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live