Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Kijaji mgeni rasmi mahafali Chuo cha Kodi

27270 KIJAJI+PIC TanzaniaWeb

Thu, 15 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Kodi yanayotarajiwa kufanyika Novemba 17, 2018.

Katika mahafali hayo wanafunzi 359 watatunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali ikiwemo astashahada, stashahada, shahada.

Akizungumza leo Alhamisi Novemba 15, 2018 na waandishi wa habari,mkuu wa chuo hicho, Profesa Isaya Jairo amesema mbali na kutunuku vyeti, wahitimu 14 pamoja na wanafunzi sita watapewa zawadi kutokana na kufanya vizuri katika masomo yao.

"Kati ya wahitimu hao 74 watatunukiwa cheti cha uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki, 33 watatunukiwa cheti cha usimamizi wa forodha ya kodi, 142 stashahada ya usimamizi wa forodha na kodi, 95 shahada ya usimamizi wa forodha na kodi na 15 stashahada ya uzamili katika kodi," Amesema Profesa Jairo.

Amesema pia wapo baadhi ya wahitimu watapewa tuzo kwa wahadhiri wa chuo hicho waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha mwaka wa masomo 2017/2018.



Chanzo: mwananchi.co.tz