Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dirisha la mikopo kujenga vituo vya mafuta vijijini kufungwa Agosti

Katibu Mkuu Wizara Ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, mhandisi Felchesmi Mramba

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kufungwa kwa dirisha la mikopo kwa wanaotaka kujenga vituo vya mafuta vijiji, Serikali imewakumbusha wafanyabishara kuchangamkia fursa hiyo ili kusogeza huduma za mafuta maeneo ya pembezoni.

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), inatekeleza programu ya kutoa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini ambapo mwisho wa kutuma maombi ni Agosti 25 mwaka huu.

Akizungumza leo Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha nishati ya mafuta inapatikana katika mazingira salama ndio sababu inafanya uwekezaji huo.

Mramba alimuwakilisha Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati wa jukwaa la mafuta na gesi lililofanyika katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba.

Akizungumza kwenye jukwaa hilo amesema Serikali inatambua umuhimu wa ushirikiano kati yake na sekta binafsi katika kufanikisha lengo la kufikisha nishati ya mafuta vijijini.

Amesema kupitia mikopo hiyo vitajengwa vituo vya mafuta vya gharama nafuu katika maeneo ya vijijini ili kuondoa madhara yasiyo salama ya usambazaji wa mafuta.

“Ushirikiano na ushiriki wa taasisi binafsi ni muhimu katika kuhakikisha tunafikia lengo la kufikisha nishati ya mafuta. REA inawezesha kuanzisha vituo vipya ya mafuta katika maeneo ya vijijini.

“Nitoe wito kwa wadau katika eneo hilo waombe mikopo ambayo Serikali ili kuwezesha kujenga vituo vya mafuta,” amesema Mramba.

Chanzo: Mwananchi