Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dili jipya biashara ya ufuta!

Ufuta Pc Data Dili jipya biashara ya ufuta!

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wameshauriwa kulima ufuta kibiashara, ili waweze kuuza ufuta wenyewe pamoja na mafuta yake.

Mratibu wa Programu ya Utafiti wa Ufuta Kitaifa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Naliendele, Joseph Nzunda alisema hayo kwenye maonesho ya Nanenane katika Viwanja ya John Mwakangale mkoani Mbeya.

Kuhusu kilimo cha ufuta alisema, mkulima akiwa na kilo 100 za ufuta akikamua mafuta atapata lita 33, na kwamba eka moja inatoa kilo 600 za ufuta.

“Kilo tatu zinatoa lita moja ya mafuta, kilo 600 ni sawa sawa na lita 200 za mafuta. Lita moja inauzwa sh 13,000 ukichukua jumla kwa eka moja unapata sh milioni 2.6.

“Maana yake hii ni biashara nzuri kwa sababu inarudisha faida zaidi ya mara mbili. Mbali na mafuta unaweza kufanya biashara ya ufuta wenyewe,” alisema.

Alishauri wakulima watumie mbegu bora kuongeza uzalishaji kwa kuwa pia ukuaji wa uchumi unategemea utumiaji wa mbegu bora.

Naye Mkurugenzi wa TARI Naliendele, Dk. Fortunus Kapinga alisema utafiti wanaoufanya unalenga kutatua changamoto katika jamii, hivyo kama watafiti wamekuwa wakiangalia jamii inataka nini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live