Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa yatekeleza miradi 41

51354 Pic+dawasa

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) imesema kipindi cha miezi sita imetekeleza miradi 41.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumanne Aprili 9, 2019 na kitengo cha mawasiliano cha Dawasa imesema zaidi asilimia 90 ya Sh15 bilioni zimetumika kutokana na vyanzo vya ndani.

"Lengo kubwa la Dawasa ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya majisafi na salama na kufikisha huduma ya maji maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam. 

"Kukamilika kwa miradi hiyo katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani kutawezesha kupunguza uwiano kwa watu wasio na huduma hiyo hasa waishio pembezoni mwa mji," imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja kuanzia leo Jumanne Aprili 9, 2019 hadi Aprili 15,  ameanza kuitembelea miradi hiyo maeneo ya Dar es Salaam, mji wa Bagamoyo na Pwani kujionea ilivyotekelezwa.

Luhemeja amesema wametenga asilimia 35 ya mapato ya kila mwezi kuwekeza kwenye miradi ya ndani na amewaagiza wakurugenzi wa idara na wakuu wa vitengo kufikia malengo waliyojiweka ili ifikapo Desemba 2019 wawe wamepunguza kero ya maji maeneo ya Dar es Salaam na miji jirani.



Chanzo: mwananchi.co.tz