Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dart yapewa miezi saba kutafuta mwekezaji mpya

Zoezi La Kuhamisha Watu Ngorongoro Kukamilika Machi   Mchengerwa.jpeg Dart yapewa miezi saba kutafuta mwekezaji mpya

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa ameielekeza Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kufikia mwezi Oktoba 2024 iwe imempata mwekezaji binafsi ambaye ni mtoa huduma wa mabasi hayo ili kuleta ufanisi.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akiwasilisha Randama ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, fungu namba 56 na fungu namba 2 la Tume ya Utumishi wa Walimu katika ukumbi wa Anne Makinda uliopo bungeni jijini Dodoma.

“Nilishawambia watu wa DART wakati wanakuja kunipitisha kwenye mfumo tunaokwenda nao ikifika mwezi Oktoba wakishindwa kuhakikisha wanampata mwekezaji atayekwenda kuhudumia njia hii wa private sekta na kushindwa kuhakikisha mabasi yamepatikana waniletee barua za kujiuzuru na tumeshakubaliana na hakuna mjadala, watu wanataka huduma,” amesema Mchengerwa

Akisisitiza hilo Mchengerwa amesema kuwepo kwa mwekezaji binafisi katika mradi huo kutafanya uendeshwe kwa ufanisi kutokana na kulipa kodi kwa serikali na wakati huohuo atawajibika endapo atatoa huduma isiyostahili.

Katika hatua nyingine, Mchengerwa amesema ifikapo Septemba hadi Oktoba serikali itakuwa imepata mabasi ya kutosha ya kuendesha njia zote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi ili wakazi wa Dar es Salaam waweze kuhudumiwa vizuri kabla ya kuanza kupeleka huduma ya mwendokasi katika majiji mengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live