Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dart kupata mbia kwenye uendeshaji

UDART DART Dart kupata mbia kwenye uendeshaji

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“DART inaendelea kukamilisha utengenezaji na usimikaji wa mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji nauli (Automated Fare Collection System-AFCS) ambao utafungamanishwa na mfumo wa kuongozea magari (Intelligent Transport System - ITS) ikiwa ni sehemu ya maboresho endelevu ya huduma hii kwa wananchi waishio mijini, na pia kuondoa mianya ya upotevu wa mapato yatokanayo na nauli.”

“ Aidha, kazi zinazoendelea kwa sasa ni usimikaji wa mageti janja (Smart turnstile gates). Vilevile, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia DART inaendelea na kazi ya kumtafuta mbia wa uendeshaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Kwanza.”

Amesema Mohammed Mchengerwa, Waziri wa Nchi OR - TAMISEMI wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live