SEPTEMBA mosi mwaka huu, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam itaanza kufanya sensa ya wiki moja kwa ajili ya kuwatambua wafanyabiashara waliopo katika eneo hilo pamoja na kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya ndani yatokanayo na tozo mbalimbali. - Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo, Jamaary Satura alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLEO kuhusu mikakati anayokusudia kuifanya ikiwa ni ndani ya mwezi mmoja tokea ahamishiwe hapo akitokea Halmashauri ya Shinyanga. - Satura alisema kwa kufanya hivyo wataweza kuwatambua wafanyabiashara wa eneo hilo kwa heshima na fedha zao, kwa kuamini wanatoa fedha ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na serikali isiende mifukoni mwa watu ambao ni makanjanja.