Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dangote kujenga kituo cha gesi asilia Dar

A50bb7cf752ebc1ba8d60fdd80a4de79 Dangote kujenga kituo cha gesi asilia Dar

Mon, 15 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIWANDA cha Saruji cha Dangote mkoani Mtwara kinatarajia kujenga kituo chake cha pili cha gesi asilia (CNG-Compressed Natura Gas) katika mkoa wa Dar es Salaam ambacho kitatumika kutoa gesi safi, salama na kwa gharama ya chini kwa malori yanayosafirisha saruji kwenda sehemu mbalimbali nchini.

Hivi karibu kiwanda hicho kilizindua kituo cha kwanza kilichopo kiwandani mkoani Mtwara chenye uwezo wa mita za ujazo 5,000 kwa saa (sawa na lita 5,000 za mafuta ( AGO-Automated Gas Oil). Kituo hicho kitatumika kutoa gesi safi, salama na kwa gharama ya chini kwa takribani malori 250.

Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akizindua kituo hicho aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa uwekezaji wa kituo hicho cha CNG.

“Nataka niwahakikishie Dangote na wale wengine wenye nia kutumia rasilimali ya gesi katika magari, serikali ipo pamoja na nyinyi kuhakikisha kwamba inaweka na kujenga mazingira wezeshi ili kaiz yah ii iwe endelevu,” alisema Waziri Kalemani.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua kituo hicho Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Dangote, Abdullahi Baba alisema malori hayo yamebadilishwa kuweza kutumia mifumo miwili yaani AGO (mafuta) na CNG (gesi asilia) kwa wakati mmoja.

“Pamoja na hayo uwezo, wa kituo hicho utatosha kusaidia katika mkakati wa kampuni juu ya matumizi ya mafuta hapo baadae ambao pia utahusisha matumizi ya gesi asilia katika malori kwa asilimia 100 katika safari zake zote,” alisema.

Akizungumzia kiwanda ambacho kitajengwa Dar es Salaam, Baba alisema kituo hicho kitajengwa jijini Dar es Salaam umbali wa kilomita 550 kutoka kilipo kiwanda cha saruji cha Dangote.

Aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ambayo yamevutia kiwanda hicho cha Dangote kuweza kuwekeza kwenye sekta ya gesi huku.

“Kwa mara nyingine tena kiwanda cha Dangote kimefungua njia katika soko kupitia utekelezaji wa teknolojia hii huku kikipata msaada mkubwa kutoka kwa serikali ya Tanzania, na kwa sasa kiwanda cha Dangote kimejipanga kuwa watumiaji wa kubwa wa pili wa gesi asilia nchini baada ya TANESCO,” alisema.

Alisema Tanzania ni kama Nigeria, imejaaliwa akiba kubwa ya gesi asilia ambapo matumizi ya gesi hii katika magari yana manufaa makubwa kifedha na kimazingira.

Chanzo: www.habarileo.co.tz