Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP World imeiongezea sifa bandari ya Dar - Makalla

Amos Makalla Msz DP World imeiongezea sifa bandari ya Dar - Makalla

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema kuwa bandari ya Dar es Salaam imeanza kuwa na sifa za kimataifa kutokana na faida za maboresho ya bandari yaliyofanyika baada ya uwekezaji wa DP World.

Makalla ameyasema hayo leo Agosti 28 alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kukagua mradi wa maboresho wa Bandari hiyo, amesema kazi imeanza kwa uboreshaji wa vifaa kwa kutoa Sh bilioni 214.425.

“Wakati wa kupata mwezeshaji kulikuwa na mjadala mkubwa na kwa tunaojua hatukushangaa kwa sababu jambo la uendeshaji wa bandari sio geni walikuwa wanasema kama vile bandari haijawahi kuendeshwa na serikali pamoja na sekta binafsi,”amesema Makalla.

Ameongeza kuwa wengi walisema uwekezaji huu utawatoa watanzania katika ajira lakini na TPA wamethibisha kuwa wafanyakazi 350 wamepata ajira kwa mwekezaji na wanaendelea kufanya kazi kuboresha bandari hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live