CHUO cha Bahari cha Dar es salaam (DMI) kimeongeza udahili kutoka wanafunzi 5,563 wa mwaka 2013/2014 hadi 9,034 kwa mwaka 2021/2022.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi was Idara ya Habari Maelezo Jijini Dodoma Dk Tumaini Gurumo amesema kuwa kuna fursa za kutosha kwenye chuo hicho vijana wazichangamkie ili wapate ujuzi na kuingia kwenye soko la ajira.
Ámesema kuwa udahili huo umeongezeka kutokana na serikali kutoa kipaumbele kwa matumizi ya vyanzo vya maji kwa maendeleo ya kiuchumi,.
“Tunatarajia kuwa na wanafunzi zaidi ya 20,000 ifikapo mwaka 2025/2026.,” Ámesema
Amesema katika mwaka wa masomo 2022/2023 DMI imedahili wanafunzi wa ngazi ya Shahada ya Pili katika jumla ya kozi tano za International Trade and Maritime Law, Shipping and Logistics Economics; Maritime Transport and Nautical Science; Marine Engineering Management na Transport and Supply Chain Management.
Amesema pia kumekuwa na ongezeko la mikopo ya wanafunzi ambapo mwaka 2021/2022 wanafunzi zaidi ya 850 walipata mkopo kulinganisha na wanafunzi 1705 walipata mkopo kwa mwaka 2022/2023.
Áidha, zaidi ya nusu ya wanafunzi waliopata mkopo wamepata kwa asilimia 100.
Amesema Chuo kinafanya tafiti na kutoa ushauri elekezi kwa serikali na taasisi binafsi.
Baadhi ya shughuli zinazofanywa ni usanifu na uandaaji wa michoro ya vyombo vya usafiri majini, ‘stability testing’, ‘inclination and tonnage testing’ na tathmini ya njia za vyombo vya majini katika vyanzo vya maji.
Ámetaja baadhi ya vyombo ambavyo DMI imevipatia huduma ni MV Kigamboni, MV. SAR IV, MV. Mwongozo, MV. Mbeya, MV. Tawa na MV. Mafia Ambulance. Ukarabati wa vifaa vya uokozi.
“Meli zaidi ya 300 zimepata huduma hii DMI zikiwemo meli zinazomilikiwa na TPA, ZPC, TRA, Azam Marine na Navy. Kuwaunganisha mabaharia na wamiliki wa meli DMI imeanza utaratibu wa kujenga uhusiano na wamiliki wa meli ili kupata nafasi za ajira na mafunzi kwa vitendo kwa ajili ya mabaharia wa Kitanzania nje na ndani ya nchi.” Ámesema