Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DIT yataka vijana kuchangamkia fursa gesi

Gaz System DIT yataka vijana kuchangamkia fursa gesi

Tue, 30 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), imewataka vijana waliopata stashahada na shahada ya uhandisi kusomea kozi fupi ya mfumo wa kuweka gesi kwenye magari ili kujiajiri na kuajiri wengine.

Hayo yalielezwa mwishoni mwa wiki na Mratibu wa Gesi Asilia wa DIT, Dk. Esebi Nyari, wakati akizungumza na gazeti hili, jijini Dar es Salaam.

Alisema vijana hao zaidi ya 300 watajifunza kufunga gesi kwenye magari na kukagua mfumo wa ukarabati huo, ili kurahisisha kasi ya kuhudumia wateja wanaoongezeka kila siku.

“Unajua mfumo huu ni mpya hapa nchini umeanza tangu mwaka 2018, ila wateja wameongezeka mwaka huu magari 350 tayari yana mfumo, hatutoi injini wala hatutoi mfumo wa kawaida wa kuweka mafuta tunaongeza kifaa kipya ili mtumiaji achague atumie gesi au petroli,” alifafanua Nyari.

Alisema kumekuwa na upungufu wa wataalamu wa kufunga mfumo wa gesi asilia kwenye magari, kutokana na kitengo hicho kuwa na mtaalamu mmoja ambaye ndiye aliyefanya utafiti na kugundua mfumo huo.

Alisema mfumo huo unatumika kwenye magari ya petroli na gharama za kuweka mfumo wa gesi kwa magari madogo yenye ‘cylinder’ nne ni Sh. 1,800,000 na ‘cylinder’ sita ni Sh. 2,200,000 na wateja wengi wanaotumia mfumo huo ni magari mtandaoni.

Alisema dereva anayetumia petroli anasafiri kilomita 12 kwa saa wakati akitumia gesi anatembea kilomita 20 kwa saa na kwamba kutumia gesi kunazuia uchafuzi wa mazingira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live