Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DHL: Uviko-19 ulifungua bidhaa za asili

Uviko Pic DHL DHL: Uviko-19 ulifungua bidhaa za asili

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DHL Express, Humprey Obace amesema wakati wa Ugonjwa wa Uviko-19 watu wengi walirudi katika matumizi ya bidhaa za asili jambo lililofungua soko la bidhaa za Tanzania zilizokuwa zikipelekwa katika masoko ya Marekani, Canada na Australia.

Kauli hiyo ameitoa leo Alhamisi, Aprili 27, 2023 katika kongamano la Wafanyabiashara wachanga, wadogo na Kati (MSMEs) lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited na kukutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya nini kifanyike ili kuwawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi.

Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam limedhaminiwa na Benki ya CRDB, Kampuni ya usafirishaji ya DHL, Benki ya Stanbic, Benki ya NMB, Clouds Media, Ukumbi wa mikutano wa Dome na Ashton

Amesema pia usafirishaji wa samaki nao uliongezeka na watu kutoka nje ya nchi walihitaji zaidi dagaa kutoka Kigoma kwani waligundua wana utajiri wa madini ya omega 3 inayosaidia kukinga mwili.

"Wakati ya Uviko-19 watu wengi walihitaji vyakula na viungo vya asili. Tuliona kuna usafirishaji mkubwa wa vitu kama dawa kutoka Tanzania kwenda Marekani, Canada na Australia," amesema

Amesema kuna fursa kubwa katika usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi na watumiaji wa soko la nje wanapata kipato zaidi kuliko wanaouza ndani.

"Mapato kutoka nje ya nchi ni makubwa kuliko yale ya soko la ndani,"

Amesema kama DHL kupitia huduma wanazotoa wamekuwa wakiwasaidia wakulima na wafanyabiashara wadogo kufika katika soko la nje.

Amesema kama kampuni inamiliki ndege 300 zinazofanya takribani safari 2400 kwa siku duniani kote.

"Si vyakula tu, pia watu wamependa aina ya nguo zinazovaliwa Afrika na tumeona hadi ‘Paris Week of Fashion’ na watu kutoka Tanzania wanaoonyesha kwa sababu ni sehemu ya Afrika," amesema

Chanzo: mwanachidigital