Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC awatimulia mbali wafugaji 'Rudini mlipotoka'

Mifugo Ya Ngombe 620x308 DC awatimulia mbali wafugaji 'Rudini mlipotoka'

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Gudluck Mlinga amewaamuru wafugaji ambao wapo katika maeneo ambayo hawakutengewa, kuondoka mara moja moja, huku akiwataka warudi walikotoka.

DC huyo ameitoa amri hiyo kwenye mkutano wa hadhara jana Jumanne Oktoba 17, 2023; katika Kata ya Kimambi, iliyopo wilayani Liwale, Mkoa wa Lindi.

Pia ameagiza kuwa mfugaji yeyote atakayeingiza mifugo kwenye shamba la mkulima, atatakiwa kulipa faini kwa wakulima wote ambao mazao yao yamewahi kuliwa na hata kama mifugo yake haikufika maeneo hayo.

"Serikali inawatambua wafugaji, tangu 2007 walitengewa maeneo katika Kata ya Kimambi, Ndapata pamoja na Lilombe, lakini hadi sasa wafugaji wameenea kwenye kata 20, na ndiyo sababu ya migogoro na wakulima," amesema Mlinga na kuongeza;

"Sasa hivi Serikali ya Wilaya ya Liwale tumeshatenga hekta 42, 000 kwa ajili ya wafugaji, bado japo bado maeneo hayo hajayapimwa...lengo la kufanya hivyo nikuondoa kabisa migogoro ya wakulima na wafugaji.”

Wakati hayo yakijiri, Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), kimewatupia lawama baadhi ya watendaji wa vijiji kikisema ndiyo chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji, kwa vile huwauzia maeneo ambayo baadaye hujikuta wako kwenye migogoro.

"Mfugaji anapoingia kwenye kijiji husika anakuwa na pesa zake, anapomuuliza mtendaji kama kuna eneo, huambiwa weka pesa mezani, matokeo yake ni muhtasari batili kuandiliwa kwa kutumia taarifa za kijiji na matokeo yake ni mfugaji kupewa eneo mahali ambapo sipo, na hapo ndipo migogoro huanza,” amesema Mwenyekiti wa CCWT Taifa, Kusundwa Wamalwa.

Hivyo basi, Makamu Mwenyekiti huyo, amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa weledi ili kuepusha migogoro kwa wakulima na wafugaji, kwani migogoro inapotokea wakati mwingine Mtendaji huamishwa huku migogoro ikibaki palepale.

"Pia, niwaombe wafugaji wenzangu kuacha tabia ya kukata kata miti hovyo, kwani kufanya hivyo ini kuharibu mazingira, tujitahidi wafugaji wenzangu kuacha tabia ya kukata kata miti, mnapo haribu mazingira mnamaliza maeneo, uzuri wa nchi yetu wote niwamoja, acheni hiyo tabia," amesema makamu mwenyekiti.

Mfugaji Hassan omary amesema kuwa watendaji ndiyo wanaosababisha migogoro, kwa kuwa wanataka hela, unapoingia kwenye eneo kwa ajili ya kutafuta makazi na malisho, wao wanakupa eneo mtaandikishiana unakuwa unamiliki eneo hilo.

"Sasa mimi nishatoa hela zangu kama milioni 3 au 4 na nimepewa eneo kutoka Serikali ya kijiji unapokuja kuniambia niondoke eneo hilo siyo langu, sitaweza kukuelewa kama wewe unamiliki kisheria, namimi namiliki kisheria, hapo ndipo migogoro inapoanzia, lakini kwa hili walilokuja nalo Serikali ya wilaya ya kutupa maeneo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro kwenye vijiji vyetu, kwa sababu wafugaji tutakuwa na maeneo yetu maalumu hatuchanganyani na wakulima," amesema Hassan.

Naye Hadija Josefu ni mkulima wa Kimambi, ameiomba Serikali kujitahidi kuwawekea miundombinu rafiki, kama ya kuwatengea maeneo yao yatakayofaa kwa ufugaji na malisho ilikuweza kuepusha migogoro ambayo inaleta maafa makubwa baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live