Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC aomba kiwanda cha chumvi

CHUMI 2 1 1024x683 DC aomba kiwanda cha chumvi

Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya ameomba kujengwa kwa kiwanda cha chumvi ili kusaidia wananchi kutumia chumvi yenye madini joto kutokana na matumizi ya madini joto kuwa chini hivyo kuhatarisha afya zao.

Ametoa rai hiyo leo mbele ya Naibu Waziri Madini, Dk Steven Kiruswa wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Uhamasishsji Uwazi na Uwajinbikaji katika rasilimali za madini mafuta na gesi asili TEIT ambapo alisema kuwa pamoja na kuwa na uvunaji mkubwa wa chumvi lakini hakuna kiwanda cha kuchakata chumvi hiyo hivyo kusababisha wananchi wengi kutumia chumvi isiyo na madini joto.

Alisema kuwa pamoja na uzalishaji wa chumvi na uwepo wa bahari bado elimu kubw inahitajika kwaajili ya kuwezesha wananchi kufahamu umuhimu wa madini joto ili waweze kuacha kutumia chumvi isiyo na madini hayo.

“Tunalo eneo kubwa la habari eneo ambalo tunafanya uwekezaji wa chumvi lakini hatuna kiwanda hali hii inachangia kushawishi wnanachi kutumia chumvi isiyostahili kiafya” alisema Kyobya

Naye Naibu Waziri Madini, Dk Steven Kiruswa amesema ombi hilo la kuwekeza kwenye viwanda vya chumvi limepokelewa na litafanyiwa kazi.

Pia, Dk Steven Kiruswa ameiagiaza TEIT kuhakikisha kuwa inaanzisha mfumo bora utakaokusanya kodi ili kubaini mchango wa sekta ya madini.

Advertisement "TEIT ianzishe mfumo bora utako saidia kukusanya kodi ili kubaini mchango wa sekta hii kikubwa zingatieni sheria za madini lipeni tozo ili ziweze kuisaidia Serikali kwenye maendeleo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live