Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC alia upotevu wa mapato migodini

FEDHA DC alia upotevu wa mapato migodini

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Sakina Mohamed amebaini uwepo wa taarifa tofauti za mapato katika vitabu vya Halmashauri ya Mbongwe na ofisi za wachimbaji wa migodi.

DC amebaini hilo katika ziara yake wilayani humo leo Jumatatu Oktoba 23, 2023, ambapo ametoa agizo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumtaka asimamie mapato halisi ya halmashauri hiyo yanayotokana na shughuli za migodi.

"Ni ajabu taarifa ya wachimbaji hapa inaonesha kuwa tangu mwaka huu wa fedha uanze wamechangia ushuru wa jumla ya Sh20 milioni kwa halmashauri yetu, wakati kwenye vitabu vya halmashauri yetu taarifa ni tofauti na inaonesha makusanyo ni madogo,” amesema.

Ameongeza kuwa, “Sasa kama huu mgodi mmoja tu taarifa yao inaonesha makusanyo yao kwa halmashauri ni Sh20 milioni tangu mwaka wa fedha huu uanze, kwa tafsiri rahisi ni kwamba migodi mingine pia imechangia kiasi kikubwa lakini hazionekani kwenye vitabu vya halmashauri yetu," amesema DC Sakina.

Mkuu huyo wa wilaya amesisitiza na kuwakumbusha watendaji wa halmashauri alioambatana nao kuwa wajibu mkubwa walio nao ni kusimamia mapato ya Halmashauri ili shughuli za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo ziendelee.

Wakati huohuo mkuu huyo wa wilaya huyo amewaonya wachimbaji wanaotorosha madini na kuwakumbusha kulipa ushuru na kodi za Serikali ni jambo la kisheria.

Amesisitiza kwamba yeyote anayetorosha madini wilayani humo hatokuwa salama kwa kuwa kamati ya usalama haitawaacha watu hao kama ambavyo ameagiza Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa wilaya hiyo pamoja na Kamati ya Usalama wilayani humo wamehitimisha ziara yao ya kutembelea na kuwasikiliza wachimbaji wa madini kwenye migodi yote ndani ya wilaya hiyo.

Ziara hiyo iliyokuwa ya siku saba amehitimisha leo kwa migodi ya Nyambogo na Shenda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live