Mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Hassan Ngoma amesema katika kuhakikisha wilaya hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali za kuleta maendeleo, amewakaribisha wawekezaji katika sekta ya madini kuwekeza, kwani sehemu kubwa ya ardhi ya wilaya hiyo ina madini.
Ngoma amesema hayo wakati wa maonesho ya madini yanayofanyika wilayani humo.
"Sisi kama wilaya tunawakaribisha wawekezaji wote kuja kuwekeza na hata kama eneo la uchimbaji lina makazi ya watu na wakawa tayari kuwalipa, sisi tutavunja ili kuhakikisha wawekezaji wanaongezeka wilayani kwetu." amesema Ngoma.
Maonesho hayo yanawakutanisha wadau wa sekta ya madini kutoka nchi kumi Duniani, yakiwa na lengo la kumulika fursa za madini zilizopo mkoani Lindi.