Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Namtumbo: Vijana mkalime, acheni kulalamika

Kilimo House DC Namtumbo: Vijana mkalime, acheni kulalamika

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo (DC), Ngollo Malenya amewataka vijana kutokaa vijiweni wakilalamika hakuna ajira na maisha magumu badala yake wajiongeze kwa kujishughulisha na kilimo.

DC Malenya amesema kilimo kinalipa na wapo waliotajirika huku akisema wilaya hiyo imepanga kufanya mapinduzi ya kilimo.

Katika kuwashawishi wananchi kushiriki kilimo amenunua na kugawa bure majembe 500 kwa wakazi wa wilaya hiyo.

"Tunataka tufanye mapinduzi ya kilimo, Rais Samia Agosti 08, 2023 alitangaza Mkoa wa Ruvuma kuwa tunaongoza kwa uzalishaji kwa hiyo Ruvuma ni 'baba' lao kwa uzalishaji wa chakula na Namtumbo tukiwemo,” amesema Malenya.

Malenya ametoa majembe hayo wakati wa Kilele cha Jukwaa la Utambuzi wa Fursa za Kilimo, Biashara na Utalii (Namtumbo Kihenge) lililofanyika Namtumbo na kuhudhuria na wadau mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live